MANCHESTER CITY YABANWA NA KULAZIMISHA SARE DHIDI YA CELTIC

 Timu ya Celtic imepata pointi yake ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuweza kutoshana nguvu na Manchester City kwa matokeo ya magoli 3-3 katika mchezo uliochezwa Glasgow.

Wenyeji waliongoza mara mbili katika kipindi cha kwanza, kupitia kwa Moussa Dembele aliyebadilisha muelekeo mpira wa kichwa wa Erik Sviatchenko na Kieran Tierney kusababisha Raheem Sterling kujifunga.

Shambulizi la Fernandinho liliifanya Manchester City kusawazisha na kisha Raheem Sterling alionekana kutulia na kufunga goli la pili, hata hivyo Dembele tena akafunga la tatu kabla ya Nolito kusawazisha.
                             Moussa Dembele akifunga goli kwa staili ya aina yake
                          Nolito akifunga goli la tatu lililoifanya City iepuke kipigo

No comments

Powered by Blogger.