Kutoka Mahakamani: Zombe Aachiwa Huru, Mwenzake Ahukumiwa Kunyongwa Hadi Kufa
Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kinondoni, SP Christopher Bageni (kushoto) baada ya kuhukumiwa kunyongwa akiagana na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Abdallah Zombe (katikati).
BAADA ya kimya kirefu, Mahakama ya Rufaa leo imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Abdallah Zombe, na maofisa wenzake wawili. Hata hivyo, mahakama hiyo imemuhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kinondoni, SP Christopher Bageni.
Bageni akielekea katika chumba maalum.
Zombe na wenzake walikuwa wakituhumiwa kuwaua wafanyabiashara watatu wa Mahenge Morogoro na teksi dereva mmoja wa jijini Dar es Salaam Januari 14, 2006 kwa madai kuwa walikuwa majambazi. Hukumu hiyo imekuja baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kutatia rufaa hukumu iliyotolewa Mahakama Kuu ya Tanzania ambayo iliwaachia huru Zombe na wenzake wanne.
Abdallah Zombe (mwenye nguo nyeupe katikati) akiwa na ndugu zake baada ya kuachiwa huru.
Wafanyabiashara wa madini waliouawa katika msitu wa Pande, wilayani Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar ni Sabinus Chigumbi maarufu kama Jongo, Mathias Linkombe, Ephrahim Chigumbi na dereva wa teksi, Juma Ndugu. Hata hivyo, DPP aliwafutia mashitaka wajibu rufani watano ambao ni Jane Andrew, Emamanuel Mabula, Michael Shonza, Abineth Salon a Festus Gwabisabi.
Post a Comment