Hamisa Mobetto amnasa mume wa Zari!
SIKU chache zilizopita mwanamitindo anayeumiza vichwa kwa sasa Hamisa Mobetto, alitupia picha katika akaunti yake ya Instagram akiwa amepiga na mume wa zamani wa Zarina Hassan, Ivan Don huko Afrika Kusini wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Starq, lakini kitendo hicho kikazua maneno kuwa tayari amemnasa mwanaume huyo.
Katika mitandao mingine ya kijamii, picha hizo zimeleta maneno mengi yasiyofaa na vijembe kwa mwanamitindo huyo akionekana kama anamchokoza Zari, kiasi cha kumfanya Hamisa kufungukia suala hilo. Zari hata hivyo hakukaa kimya baada ya tukio hilo, naye katika mtandao wake, akatoa maneno ya kejeli, akibeza picha hizo na kudai mtu asipokutangaza hadharani kama wewe ni mtu wake, ujue hauna lolote.Jamani Hamisa, wakati bado mwenzake anamuona katembea na mzazi mwenzake Diamond, bado tu anamchokonoa, hii siyo sawa kabisa, alisema mmoja wa wachangiaji katika mtandao huo. Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Hamisa ili kuweza kujibu tuhuma hizo ambapo alisema Ivan, alikuwa ni mmoja wa washiriki katika tuzo hizo na walipiga picha kawaida tu, lakini anawashangaa watu wanachulia kivingine. Jamani mimi nafikiri kila mtu na uelewa wake, kuna tatizo gani mtu kupiga picha na mshindi mwenzako kwa sababu wao kundi lao la Money Gang lilishinda na mimi nikashinda tuzo yangu ya Uvaaji Bora wa Mwaka kwa mwanamke, lakini watu wanachukua vitu ndivyo sivyo mpaka wananichosha mimi, alisema Hamisa.
Post a Comment