Dayna Nyange Nalitamani Penzi La Idris

 Staa wa Bongo Fleva, Mwanaisha Said ‘Dayna Nyange’.

Makala: Boniphace Ngumije
NAAM ni siku nyingine tena tumekutana katika kona yetu hii ya Mtu Kati. Baada ya wiki iliyopita katika kona hii kuwaletea msanii kutoka Bongo Muvi, Ester Kiama leo tumegeukia kwa upande wa Muziki wa Bongo Fleva na kumpata Mwanaisha Said ‘Dayna Nyange’. Dayna ni mmoja wa mastaa wa kike Bongo aliyejipatia umaarufu kupitia ngoma kibao kama Mafungu ya Nyanya, Angejua na sasa anatamba na Ngoma ya Komela. Makala haya, yanahusu maisha yake kimuziki na nje ya muziki;
                                              Mshindi wa Big brother Africa 2014 Idris Sultan.
Mtu Kati: Ujio wako mpya sokoni umepokelewa vipi na mpaka sasa umekupa mafanikio gani? Dayna: Ujio wangu ambao ni Wimbo wa Komela, nashukuru Mungu umepokelewa vizuri ukiangalia hauna video lakini umekuwa na manufaa makubwa kwangu kwani umenipa connection za kutosha.
Mtu Kati: Unaweza kutaja mambo matatu ambayo huwezi kuyasahau katika maisha yako?
Dayna: La kwanza ni siku ambayo nilimpoteza shangazi yangu ambaye alikuwa kama mlezi wangu kwa miaka 21. Pili siku ya kwanza kuitwa mama kwani nilibadilika kabisa kimaisha na tatu ni siku baada ya kutambua kuwa nimekuwa mtu ambaye naweza kufanya kitu chochote kikaniingizia pesa na kuweza kumiliki vitu vyangu mwenyewe.
Dayna Nyange akiwa katika pozi.
KUBANJUKA NA MASTAA WENZAKE VEPEE? Mtu Kati: Kuna tetesi kuwa umeshawahi kubanjuka na wasanii wenzako?
Dayna: Hahaaa! Kwa hilo hapana, sijawahi na wala sitarajii kuja kutoka kimapenzi na msanii mwenzangu.
HEE! IDRIS NAYE? Mtu Kati: Umewahi kuvutiwa na staa gani Bongo kimapenzi?
Dayna: Dah! Nilishawahi kusema ikazua mushkheri kidogo, ukweli ni kwamba Idris (wa BBA) ni mtu ninayempenda na kumtamani sana sana sana! Namuangalia, namfuatilia na kumheshimu sana.
Ni mtu ambaye nikikaa naye siboreki kabisaaa. Ni mtu ambaye akiamua kufanya tukio anafanya kifupi anasimama katika msimamo wake, natamani penzi lake.
                                   Idris Sultan akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Wema Sepetu.  KUFUMANIWA JE?
Mtu Kati: Umewahi kufumania ama kufumaniwa na mpenzi wako?
Dayna: Kiukweli katika maisha ya mapenzi kinachotukosti sana ni wivu. Nilishawahi kufumania meseji yakaisha lakini siyo kumfumania na mwanamke.
Mtu Kati: Umewahi kupokea kipigo kutoka kwa mpenzi wako na sababu ilikuwa ni nini?
Dayna: Kukosea ipo japo unapigwa kidogo kakofi  ka mapenzi lakini sijawahi kabisa kupokea kile kipigo na kusababisha kuumia sana.
ANACHOMISI KWA ‘MUPENZI!’
 Mtu Kati: Huwa unamisi nini zaidi ukiwa mbali na mpenzi wako? Dayna: Namisi vingi yaani namisi vyote vinavyotakiwa kumisiwa na mpenzi wako kama alikuwa akipenda kunikisi nitamisi.

Mtu Kati: Umewahi kuingia bifu na msanii yeyote ndani na nje ya nchi na chanzo kilikuwa nini?
Dayna: Ni kweli nilikuwa na mzozo na Diamond lakini sitaki tena turudi kule tulipoto-kea kwani yaliisha.
KUSHINDA NJAA JE? Mtu Kati: Katika maisha yako, umewahi kushinda ama kulala na njaa kwa kukosa pesa?
Dayna: Inatokea lakini kutokana na majukumu, siku hizi watu tunaishi vizuri na majirani na marafi ki, sasa huwezi kushinda na njaa hapa mjini na majirani wanakutazama tu. Ila unaweza kukwama kwa kushindwa kununua pamba kwa kuwa fasheni mpya imetoka. Makala: Boniphace Ngumije
Mtu Kati: Unapenda kuwa na mwanaume wa aina gani?
Dayna: Swali gumu lakini nilikuwa napenda sana wanaume wale wa kimya (wa pole) lakini mwisho wa siku ukija kumfungulia boksi unakutana na tabia za hatarihatari.
Mtu Kati: Unaweza kumuweka wazi mwanaume unayetoka naye kwa sasa? Dayna: Siwezi kufanya hivyo kwa kwa sababu sihitaji kuharibu uhusiano wangu wa sasa.
Mtu Kati: Inajulikana una mtoto, kipi hupendi mwanao afahamu kuhusu wewe? Dayna: Sipendi ajue uhusiano wangu kwa sasa. Sipendi mwanangu ajue kabisa kama natoka na nani. Nilivyomlea najua mwenyewe, uhusiano halali ni ule wa ndoa tu.
MASTAA WENZAKO VEPEE?
Mtu Kati: Kuna tabia yoyote unaichukia kutoka kwa wanamuziki wenzako wa kike?
Dayna: Zipo nyingi tu lakini siwezi kuziongela kwa sababu ni maisha ya mtu binafsi na uamuzi wake. Hata mimi huenda kuna msanii mwenzangu namkwaza. Mtu Kati: Unatengeneza vipi pesa kupitia muziki?
Dayna: Kupitia shoo, matangazo na ishu yoyote inayohusiana na muziki. Ukiangalia wasanii wengi wa kike nilioanza nao wameishia njiani.

No comments

Powered by Blogger.