CRISTIANO RONALDO ACHUKIZWA KUTOLEWA NJE WAKATI REAL MADRID IKITOKA SARE

Cristiano Ronaldo amechukizwa na kitendo cha kutolewa uwanjani na kocha Zinedine Zidane kabla ya mpira kumalizika katika mchezo ambao Real Madrid ilitoka sare ya magoli 2-2 na Las Palmas.

Mchezaji huyo bora wa mwaka wa Fifa mara mbili, alitolewa katika dakika ya 72, ikiwa ni mara ya kwanza kubadilishwa ili aingie mchezaji mwingine katika kipindi chake cha miaka saba ya soka.

Kocha Zidane alimpatia mkono Ronaldo ambaye alipata wakati mgumu kukubaliana na maamuzi hayo, lakini mshambuliaji huyo mreno hakutaka hata kuangaliana usoni na kucha wake huyo wa Real Madrid.
 Cristiano Ronaldo akipeana mkono na kocha Zidane bila ya kumuangalia baada ya kuchukizwa na uamuzi wake wa kumtoa nje
              Karim Benzema akishangilia goli alilofunga akiwa na Gareth Bale

No comments

Powered by Blogger.