Waziri Mwinyi: Mipaka ya Tanzania iko Salama.
Na: Lilian Lundo- Maelezo
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi
amewahakikishia watanzania kwamba mipaka ya Tanzania ni salama.
Mhe.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo katika kipindi cha Tunatekeleza
kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC) alipokuwa akieleza mikakati
ya wizara hiyo katika kuhakikisha mipaka ya Tanzania iko salama.
“Nchi
iko salama, mipaka ya nchi iko shwari, ziko changamoto chache za nchi
zinazotuzunguka kuwepo katika machafuko mfano Burundi hivyo wananchi
wake kukimbilia Tanzania,” alifafanua Mhe. Dkt. Mwinyi.
Amesema
Tanzania sio kisiwa, imejiunga na jumuiya mbali mbali kama Jumuiya ya
Afrika Mashariki, Jumuiya ya Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Umoja wa
Mataifa hivyo kupitia Jumuiya hizo Tanzania hupata maelekezo ya
kuwapokea wakimbizi kutoka nchi zenye machafuko.
Hata
hivyo Mhe. Dkt. Mwinyi amesema kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inahakikisha wakimbizi wanaoingia
nchini wanafuata utaratibu unaotakiwa bila kuvunja sheria za nchi.
Pia
ameeleza kuwa Tanzania inaendelea na mazungumzo ya amani na nchi ya
Malawi juu ya mgogoro wa umiliki wa Ziwa Nyasa baina ya nchi hizo mbili
ili kupata ufumbuzi wa amani, ambapo mazungumzo hayo ya yanaongozwa na
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William
Mkapa.
Aidha,
Mhe. Dkt. Mwinyi amesema kuwa kutokana na Wizara hiyo kufanya vizuri
katika Ulinzi na Amani ya Nchi, Jumuiya ya Umoja wa Afrika na Jumuiya ya
Umoja wa Mataifa imeiomba nchi ya Tanzania kutoa Ulinzi wa Amani kwa
nchi za Sudani, Kongo na Lebanoni kutokana na machuko yanayoendelea
katika nchi hizo.
Vile
vile ameeleza kuwa, ushiriki wa Jeshi la Tanzania katika nchi zenye
machafuko kunaisaidia Jeshi hilo kupata mafunzo ya kivita kutokana na
Tanzania kuwa ni nchi ya amani hivyo kufanya baadhi ya wanajeshi
kutoshiriki mafunzo ya uhalisia ya kivita tangu wanapoajiriwa mpaka
kustaafu.
Post a Comment