WANAFUNZI 80 MKOANI KILIMANJARO WASIMAMISHWA MASOMO KWA UJAUZITO
WANFUNZI 80 wa shule za msingi na sekondari mkoani
Kilimanjaro wamesimamishwa masomo katika kipindi cha kuanzia mwezi January hadi
Julai mwaka huu baada ya kubainika kuwa na ujauzito.
Afisa elimu mkoa wa Kilimanjaro Bi Euprasia Buchuma
amemweleza Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia kuwa tatizo la ujauzito kwa
wanafunzi mkoani Kilimanjaro ni kubwa hali ambayo inasababisha kiwango cha
ufaulu kwa wanafunzi wa kike kushuka kila mwaka.
Amesema tatizo hilo limeonekana kubwa baada ya agizo la Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro kutaka wanafunzi wakike wapime ujauzito wakati wanarudi
mashuleni baada ya kumaliza likizo na kwamba muamko wa jamii kuwachukulia hatua
wale wanaowabebesaha wanafunzi ujauzito ni mdogo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw.Saidi Meck
Sadick amesema wilaya ya Rombo inaongoza kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi 22
wenye ujauzito ikifuatiwa na wilaya ya Siha wanafunzi 12,Hai 11 huku wilaya ya
Same ikiwa haijabainika kuwa na mwanafunzi wa kike mwenye ujauzito.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako
amewaagiza maafisa elimu nchini kuhakiki taarifa za wanafunzi hewa na kwamba
kwa wilaya au mkoa utakayobainika kuwa na wanafunzi hewa Afisa Elimu husika
atawajibishwa.
Post a Comment