PLUIJM: NANI ANASEMA TUMEKATA TAMAA, KWA NINI TUKATE TAMAA?
Kocha Hans van der Pluijm amesema kikosi chake hakijakata tamaa katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
Pluijm
raia wa Uholanzi, amesema bado wanapambana na watakachofanya ni kuibuka
na ushindi dhidi ya Bejaia ambayo iliwafunga bao 1-0 kwao Algeria.
“Mechi
itakuwa ngumu, lakini katika soka hauwezi kukata tamaa mapema tena kwa
rahisi namna hiyo. Kama tutashinda, basi tuna nafasi bado,” alisema
Pluijm.
Kikosi
cha Yanga kimeendelea na mazoezi yake kabla ya kuiva Mo Bejaia ya
Algeria katika mechi ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa,
Jumamosi.
Yanga imefanya mazoezi yake ya mwisho kwenye uwanja huo leo kabla ya mechi hiyo ya Jumamosi.
Post a Comment