Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(kulia) akimkabidhi mpira Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,
Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga ikiwa ni ishara ya Naibu Waziri huyo
kuzindua Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Waendesha Pikipiki katika Mkoa
wa Kipolisi wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo
yajulikanayo kwa jina la Mpinga CUP yanatarajiwa kuanza kesho jijini
humo. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka waendesha Boda Boda jijini
humo na nchini kwa ujumla kufuata sheria za usalama barabarani, na pia
elimu ambayo wanapewa waitumie vizuri ili kuepuka ajali mbalimbali
zinazosababishwa na uzembe wa madereva hao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akizungumza na waendesha Pikipiki/Boda Boda (hawapo pichani) kabla ya
kuzindua Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Waendesha Pikipiki katika Mkoa
wa Kipolisi wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo
yajulikanayo kwa jina la Mpinga CUP yanatarajiwa kuanza kesho jijini
humo. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka waendesha Boda Boda jijini
humo na nchini kwa ujumla kufuata sheria za usalama barabarani, na pia
elimu ambayo wanapewa waitumie vizuri ili kuepuka ajali mbalimbali
zinazosababishwa na uzembe wa madereva hao. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi
cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Kulia ni
Wafadhili wa Mashindano hayo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(aliyevaa koti) akimsikiliza Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani
nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga wakati alipokuwa anazungumza na
Waendesha Boda Boda (hawapo pichani), kabla ya Naibu Waziri Masauni
kuzindua Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Waendesha Pikipiki katika Mkoa
wa Kipolisi wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Kamanda
Mpinga alisema Mashindano hayo ambayo yameshirikisha Wilaya za Temeke,
Kinondoni na sasa Ilala yanatarajiwa kumalizika Septemba 18, 2016.
Post a Comment