MTOTO WA OBAMA AONDOKA IKULU, AAMUA KUWA MHUDUMU WA MGAHAWA
Sasha Obama
akihudumia mgahawani.
Marekani
Marekani
IKIWA imebaki miezi
miwili tu ili utawala wa Rais wa Marekani Barack Obama ufikie ukomo, binti
mdogo wa rais huyo mwenye asili ya Kenya, Sasha Obama ameamua kuacha ‘starehe’
za Ikulu ya White House na kuondoka kwenda kufanya kazi katika mgahawa mmoja,
vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti.
Mgahawa anapofanya kazi mtoto wa rais Obama
Sasha mwenye umri wa miaka 15 ameanza kufanya kazi ya
kuwahudumia wateja katika mgahawa mmoja ulioko Martha’s Vineyard, Massachusetts
na picha zilizopigwa zinamuonesha akiwa amevalia sare za kazi za hoteli hiyo na
akifanya kazi.
Sasha Obama.
Binti Sasha ambaye anatumia jina lake kamili, Natasha,
aliandamana na maafisa sita wa ulinzi wa secret service siku yake ya kwanza
kazini, gazeti la Boston Herald linaripoti.
Menu ya mgahawa huo.
Taarifa zilizochapishwa na gazeti hilo zinaeleza kuwa
familia ya ais Obama hutembelea eneo hilo mara kwa mara wakati wa likizo.
Mfanyakazi mmoja katika mgahawa huo aliambia gazeti la
Herald: “Tulikuwa tunashangaa ni kwa nini kulikuwa na watu sita walikuwa
wanamlinda binti huyu, lakini baadaye tukagundua alikuwa nani (mtoto wa rais
Obama).”
Post a Comment