Mahakama Kuu yatengua hukumu ya awali ya kuwafutia shtaka la utakatishaji fedha aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Kitilya na wenzake
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetengua uamuzi uliotolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Emmilius Mchauru wa kufuta shtaka la kutakatisha Dola Milioni 6 za Kimarekani baada ya kuona liliondolewa kinyume cha sheria!
Kesi
hiyo inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) (pichani kati) Harry Kitilya na wenzake dhidi ya mashtaka manane
ikiwamo la kutakatisha fedha na walipandishwa kizimbani kwa mara ya
kwanza Aprili Mosi Mwaka huu.
Akisoma
uamuzi huo Jaji Edson Mkasimongwa alisema baada ya kupitia hoja za
pande zote mbili mahakama yake imeona Hakimu Mchauru wa Mahakama ya
Kisutu alikosea kuliondoa shtaka hilo na kwamba shtaka la kutakatisha
fedha litabaki kama lilivyofunguliwa katika hati ya mashtaka.
"mahakama
ya Kisutu ilikosea kisheria kulifuta shtaka la 8 na ninaamuru kurejesha
kumbukumbuku ya jalada la kesi hii kwa ajili ya kuendelea kusikilozwa"
alisema Jaji Mkasimongwa.
Mbali
na Kitilya washtakiwa wengine ni Miss Tanzania 1996 Shose Sinare na
Sioi Solomon ambao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi
Mchauru.
Awali,
jopo la mawakili wa utetezi liliwasilisha maombi ya kuliondoa shtaka la
nane ya kutakatisha fedha na mahaka?a ya Kisutu ilikubali na kuliondoa.
Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Osward Tibabyekomya ulowasilisha nia ya kukata rufaa kupinga uamuzi huo.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Dar es Salaam alitupilia mbali rufaa hiyo
baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kwamba mahakama yake haina
mamlaka ya kusikiliza rufaa ya kuondolewa shtaka la kutakatisha fedha.
Upande wa Jamhuri ulikata rufani katika Mahakama ya Rufani Tanzania.
Mahakama
hiyo iliyoketi chini ya Jopo la Majaji watatu ikiongozwa na Bernad
Luanda,Salum Masati na Aristoclas Kaijage liliamuru jalada la kesi hiyo
kurejeshwa mahakama kuu na kupangiwa jaji mwingine wa kusikiliza rufaa
ya Jamhuri.
Jalada hilo lilipangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Mkasimongwa.
Post a Comment