IDRIS SULTAN NA WEMA SEPETU WAZINGUANA TENA
Idris Sultan
na Wema Sepetu wamezinguana kwa mara nyingine tena.Kisa na mkasa ni Wema
kuisusia show ya Idris, Funny Fellas kwa mara nyingine tena huku mshindi huyo
wa Big Brother akihudhuria za mpenziwe, ikiwemo Black and Tie iliyofanyika
mwezi uliopita.Baada ya kuchoshwa na tabia ya mpenzi wake kutompa support
kwenye show zake, Idris naye aliamua kuipotezea show ya Usiku wa Vigoma
iliyoandaliwa na Sepetunga mwishoni mwa wiki – na hapo ndipo mambo
yalipoharibika. Mashabiki wa Wema wamekasirika baada ya shemeji yao kuikwepa
show hiyo na wanamshambulia Instagram. Kutokana na kuandamwa,
Idris amelazimika kuongea:
"Sipendi
kuona watu wakiingia na kuongea kama wanajua maisha yangu na watu wangu wa
karibu, makosa wakifanya wengine mnakuja kwangu mnaanza “Ndio asingefanya vile
kama sio wewe kufanya hivi” mnakazana kusema eti naposti wanawake mara ooo
porojo kibao. Sina freedom ya kumpost dada angu ? Kweli ? Au rafiki yangu
kazindua brand mpya siwezi mpost nikampongeza? Mnauliza kwanini sijaenda vigoma
nimesema because show yangu hakuja hata moja na nimeenda show zake zote na yeye
halalamiki because anajua nimesema siendi fair enough mbona hamjaongelea hilo?
I repeat nikikaa kimya is for a pure reason that it’s not anyones business this
is my personal life kama mnaongeleaga fair basi mngefanya kuuliza kwanini mpaka
am selling out hajaja.Give me a break sina maisha ya kuigiza lets have respect
for each other bana. Na nimesema msiniite shemeji for one big good reason,
imekua too much i am a brand na jina idris linamezwa na shem, ningejua this
from the beginning nisingeruhusu mniite tangu mwanzo so msiwe kila kitu
mnafikiria negative tu. Na sikuwa na haja ya kuandika yote haya pia
TusichukulianePoa.
Post a Comment