EXCLUSIVE: MANJI ATANGAZA KUOMBA KUIKODISHA TIMU YA YANGA KWA ASILIMIA 75 WANACHAMA WAKUBALI, WAMPA

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amekata kiu ya kile ambacho wanachama wengi na wapenda soka nchini walikuwa wakikisubiri kwenye mkutano wa dharura aliouitisha.

Baada ya kujadili, wanachama wa Yanga pamoja na wajumbe wa bodi wakapitisha kumkodisha Manji kwa miaka kumi kama alivyoomba.

Katika mkutano huo unaofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam kipindi hiki, Manji amesema amepeleka ombi la kuikodisha Yanga kwa miaka 10.

“Nitaikodisha kwa asilimia 75 na 25 inabaki kwa wanachama. Nataka kuikodisha timu na nembo, majengo ya klabu yanabaki kuwa mali ya wanachama.

“Katika miaka 10, ikipatikana faida 25 inakwenda kwa wanachama na klabu na 75 kwangu. Kama itakuwa ni hasara basi inakuwa hasara yangu, hakuna hasara upande wa wanachama au klabu,” alisema.

“Tayari nimewasilisha ombi hilo Bodi ya Wadhamini ambao wao watazungumza na nyinyi wanachama na kama kutakuwa na makubaliano basi tutaingia mkataba,” alisema Manji.


Manji alisema masuala ya timu kuhusu usajili, mishahara, uendeshaji kama safari na gharama nyingine zitakuwa chini yake.

Pia asilimia 25 ambayo itakuwa ni ya klabu, ndiyo itatumika kuujenga Uwanja wa Kaunda na Yanga itakuwa na uwanja wa kufanyia mazoezi na ikiwezekana hata kuchezea mechi.

Wanachama wengi walionekana kufurahi na wengi walisisitiza kwamba wanakubali hata kabla ya kuanza kwa mchakato huo rasmi.
06 Aug 2016

No comments

Powered by Blogger.