Pluijm: Yanga Waje, Tunaanza na Azam

                                                          Kikosi cha timu ya Yanga.
KOCHA wa Singida United, Hans van Der Pluijm amesema hana wasiwasi kupangwa na Yanga katika robo fainali ya Kombe la FA lakini anataka kuifunga Azam FC kwanza katika Ligi Kuu Bara.

Leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam, Azam itakuwa mwenyeji wa Singida United katika mechi ya ligi kuu inayotarajiwa kuwa ngumu.

Azam ipo nafasi ya tatu katika ligi ikiwa na pointi 35 huku Singida United ikiwa nafasi ya nne na pointi 34, hivyo mshindi anaweza kujiimarisha zaidi katika msimamo.

Pluijm ameliambia Championi Jumamosi kuwa: “Tunafahamu ubora wa Azam, tutatilia mkazo zaidi katika mechi hiyo na tunaamini tutatengeneza nafasi zaidi za kujipatia ushindi.”

Akizungumzia ratiba ya mechi za robo fainali za Kombe la FA iliyopangwa jana ambapo watacheza na Yanga ambayo amewahi kuifundisha, Pluijm alisema, hawana wasiwasi kwani anaijua timu hiyo vizuri.

“Sina wasiwasi na ratiba kwani Yanga naijua, tunajitengenezea mazingira ya ushindi ili tujiweke katika nafasi ya kupata tiketi ya mechi za kimataifa msimu ujao,” alisema Pluijm raia wa Uholanzi.

Bingwa wa Kombe la FA anapata nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika huku bingwa wa ligi kuu akishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika
Stori: Khadija Mngwai na Ibrahim Mussa

No comments

Powered by Blogger.