Rais Magufuli akataa ombi la kuongoza miaka 20
Baada ya Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani (Profesa Maji Marefu) kuomba Rais Magufuli aongoze miaka mingine 10 ya kuongoza ili atawale nchi kwa miaka 20 . Rais Magufuli amesema suala la yeye kuongoza miaka hiyo haliwezekani.
Prof. Maji marefu amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa standi mpya ya mabasi iliyopo katika halmashauri ya mji wa Korogwe ambapo amedai kuwa Rais Magufuli anafanya kazi ambayo Watanzania wanaipenda na inaonekana hivyo itakuwa ni jambo jema kama ataongezewa muda zaidi ya kuongoza.
“Ndio maana hapa mtani wangu ulipozungumza hapa kwamba unataka miaka 20 zaidi nilielewa kwamba unataka niishi miaka 20 zaidi sio miaka 20 ya Urais hilo haliwezekani kwasababu nitaheshimu Katiba na hii kazi ngumu, kutumbua majipu mengine yameoza yanakurukia mdomoni unaweza shindwa hata kwenda kula, ni kazi ngumu ni kazi ambayo ni very risk lakini ni lazima ninyame kwa niaba ya Tanzania kwasababu nisipo tumbua nani atakuja kutumbua?,” amesema na kuhoji Rais Magufuli.
Siku ya Eid El Fitr, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Tanzania, Mh Ally Hassan Mwinyi Mhe. Mwinyi akitoa salamu za katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam isingekuwa Katiba, ningetamani Rais huyo aongoze siku zote.
Post a Comment