MAWAZIRI WAMPANDA KICHWANI DKT SHEIN, AAHIDI KULA NAO SAHANI MOJA
Rais Dkt. Ali Mohamed Shein akisaini kitabu cha wageni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, ametoa onyo kwa mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambao hawakuhuduria katika Ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
Dkt. Shein akizungumza na viongozi, katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud.Dkt Shein ameyasema hayo leo baada ya kupokea ripoti ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyowasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani, ambapo baada ya kuwasili akakuta idadi chache ya mawaziri, kitendo kilichomkasirisha, na kuonekana kwamba wamekiuka amri yake au kudharau ziara yake ambayo ina maslahi kwa Zanzibar.
Rais akikagua miradi.
“Baadhi ya mawaziri wangu hawapo, narudia tena leo, nataka niwaone mawaziri wangu katika ziara hii, wapo wawili wameniaga, wengine hawajaniaga, nilisema juzi pale Tunguu, narudia tena hii siyo ziara ya mchezo, hii ni ziara ya kazi, wanayoyatafuta wakitaka watayapata, “ amesema Dkt Shein.
Miradi ya ujenzi ikiendelea.
Dkt Shein ameanza rasmi leo, ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika mkoa wa mjii magharibi, ambapo amekagua shughuli za ujenzi wa kiwanja cha michezo kilichopo Kikwajuni uwanja wa Mao, pia amekagua mradi wa kasi ya mawimbi ya bahari, katika maeneo ya Kilimani- Kizingo, ameweka jiwe la msingi katika jengo la chuo cha utalii Maruhubi.
Rais akikagua miradi.
Pia amehitimisha ziara yake kwa siku ya leo, kwa kuzindua Tawi la CCM, Mwembe Matarumbeta lililopo katika Jimbo la Jang’ombe, ambalo liliwahi kuungua moto mwaka 2014 katika kipindi cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
Wafuasi wa CCM wakicheza.
Rais Dkt Shein anatarajia kuendelea tena na ziara yake hapo kesho, ambapo atahitimisha siku ya Jumatatu.
Post a Comment