timu ya Athletic Bilbao yaifanyia kufuru timu ya samatta

MSHAMBULIAJI mkongwe raia wa Hispania anayekipiga Athletic Bilbao  Aritz Aduriz amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matano kwenye michuano ya  Europa miamba hiyo ikiiua KRC Genk anayochezea Mtanzania Mbwana Samatta mabao 5-3.
Aduriz mwenye miaka 35 alifunga hat-trick kwa penalti na kuwa Mhispania wa kwanza kufunga mabao matano kwenye michuano ya Ulaya tangu mwaka 1971.

Kwenye mchezo uliopita Genk waliwachapa Bilbao mabao 2-0 kwenye ardhi yake ya nyumbani huku Samatta akiingia kutokea benchi baada ya kutoka kwenye majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua.

Mabao ya Genk yalifungwa na Leon Bailey, Onyinye Ndidi pamoja na Tino-Sven Susic.

Matokeo mengine ya mechi za Europa FC Astana 1-1 Olympiacos Anderlecht 6-1 Mainz 05 Sasuolo 2-2 Rapid Wien Fenerbache 2-1 Man United FC Astra 1-1 Victoria Plzen FC Zenit 2-1 Dundalk Zorya 1-1 Feyernood Austria Wien 2-4 As Roma FK Qabala 1-2 Saint Etienne

No comments

Powered by Blogger.