OKWI NDANI, ORLANDO PIRATES YAITWANGA SIMBA KWA BAO 1-0
Simba imechapwa kwa bao 1-0 katika mechi yake ya kwanza ya kirafiki baada ya maandalizi ya msimu wa 2017-18.
Simba imelala kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wake Orlando Pirates katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Orlando jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Mganda Emmanuel Okwi na John Bocco ndiyo walioongoza mashambulizi na walifanya kila juhudi kutaka kusawazisha bao hilo lililofungwa katika kipindi cha kwanza lakini hawakufua dafu dhidi ya vigogo hao wa Afrika Kusini.
Post a Comment