Mkuu wa Wizara ya Pasipoti za Ndani na Shirika la Uandikishaji wa Raia wa Jamhuri ya Sudani atembelea Idara ya Uhamiaji Tanzania

 Mkuu wa Wizara ya Paspoti za Ndani na Shirika la Uandikishaji wa Raia wa Jamhuri ya Sudan, Luteni Jenerali Awad Al Neil Dahia, (katikati) akikabidhi hedaya kwa Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Hannelore M. Manyanga, baada ya kikao ambacho Maafisa Uhamiaji toka Vitengo vya TEHEMA na Udhibiti wa Mipaka waliwasilisha mbinu anuai za kudhibiti Wahamiaji.
 Naibu Kamishna wa Uhamiaji,Fulgence Mutarasha, Mfawidhi wa Kituo cha Uhamiaji Uwanja wa Ndege Mwl. JK Nyerere akitoa maelezo ya Utendaji wa Shughuli za Kiuhamiaji kwa mgeni wake, Mkuu wa Wizara ya Paspoti za Ndani na Shirika la Uandikishaji wa Raia wa Jamhuri ya Sudan, Luteni Jenerali Awad Al Neil Dahia, (katikati)  ambaye alisindikizwa na Maafisa toka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Shirika la Uhamiaji
la Kimataifa, IOM, Tanzania. 
Mkuu wa Wizara ya Paspoti za Ndani na Shirika la Uandikishaji wa Raia wa Jamhuri ya Sudan, Luteni Jenerali Awad Al Neil Dahia, (katikati)  akipitishwa eneo la Kuwasili Abilia ndani ya Uwanja wa Ndege Mwl. J.K Nyerere alipotembelea Kituo cha Uhamiaji uwanjani hapo  kujifunza shughuli za Uhamiaji Tanzania.

No comments

Powered by Blogger.