Mbaraka Yusuph atangaza vita


                                                                           Mshambuliaji Mbaraka Yusuph.

Ikiwa zimebakia siku chache vumbi kuanza kutimka katika mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Mshambuliaji mpya wa Mabingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Mbaraka Yusuph ameahidi kufanya makubwa katika michuano hiyo hasa upande wa mchezaji bora. 
Mbaraka ametoa kauli hiyo hivi karibuni baada ya kujiunga na timu hiyo na kudai alikuwa na ndoto ya muda mrefu kujiunga na miamba hiyo ya soka Afrika Mashariki na Kati.
“Kwa kweli nimejipanga kufanya vizuri zaidi kuliko msimu uliopita, natarajia Mwenyezi Mungu akinijalia kila mechi nitakayocheza niweze kupata nafasi, niweze kufunga na kuwa mfungaji bora wa ligi”, alisema Mbaraka.
             Mbaraka Yusuph akiwa anafanya mazoezi katika klabu yake ya Azam FC.
Kulingana na kauli hiyo ni wazi Mbaraka ametangaza vita kwa baadhi ya wachezaji wa vilabu vingine ambao walifanya vyema katika msimu wa Ligi Kuu Bara uliopita ambapo Shiza Kichuya (Simba) alitwaa tuzo ya Goli Bora la Msimu, Mohamed Hussein Hussein 'Tshabalala' a.k.a Zimbwe Jr (Simba)  aliweza kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Vita hiyo aliyotangaza Mbaraka inaweza kuwa ngumu zaidi kwa msimu huu mpya kutokana na klabu nyingi kuwa na wachezaji wazuri ambao wengi wao wana malengo ya kuhakikisha wanashinda na kuibuka na heshima na tuzo mbalimbali, hali ambayo inaweza kuleta ushindani mkubwa zaidi. 
Kwa upande mwingine, Mbaraka Yusuph amesaini kandarasi ya miaka miwili kuwatumikia wanarambaramba hao wa vingunguti huku akiwa shabiki mkubwa wa staa wa Baracelona na Argentina, Lionel Messi,

No comments

Powered by Blogger.