Binti wa Chuo Kikuu cha Makumira Adaiwa Kubakwa Hadi Kufa Kisha Mwili Wake Kutupwa
INASIKITISHA SANA: Binti mmoja ambaye ni model na
mwimbaji wa muziki aliyetambulika kwa jina la JULIANA ISAWAFO (pichani)
ambaye picha yake ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia jana
ikionyesha mwili wake ukiwa umetupwa eneo la Ndoro nje kidogo ya Chuo
Kikuu cha Makumira, Arusha baada ya kudaiwa kubakwa na watu
wasiojulikana.
Mmoja wa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho, (jina lake
halikufahamika mara moja) amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na
kusema kuwa ameokotwa majira ya saa tano asubuhi jana akiwa amekufa na
mwili wake kutelekezwa kwenye shamba la mpunga nje kidogo ya eneo la
chuo hicho.Mbali na kuthibitisha kifo hicho, kiongozi huyo ameeleza pia kuwa, msichana huyo ni mwanafamilia wa Chuo cha Makumira ila hakuwa mwanafunzi rasmi kama watu wanavyodai.
chanzo:matandao wa globalpubrishers
Post a Comment