Masauni: Polisi, Temesa na NIT kuungana kukagua magari nchini
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyekaa), akimsikiliza rubani Edger Mcha (kulia) wa Chuo cha Usafirishaji nchini (NIT) kilichopo jijini Dar es Salaam, wakati alipokua anamuonyesha jinsi ya kuongoza ndege inapotaka kuruka na kutua kutoka katika kiwanja cha ndege. Mwenyekiti huyo alipata maelezo hayo wakati alipokua katika darasa la kufundishia marubani chuoni hapo. Masauni alifanya ziara katika chuo hicho na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kwa lengo la kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini. Akiwa chuoni hapo aliangalia ukaguzi wa magari na pia kupata mipango mbalimbali waliyonayo kuhusiana na elimu wanayoitoa ya kuhusiana na usalama barabarani. Aliyevaa koti ni Mkuu wa Chuo hicho, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza hilo, Profesa Zakaria Mganilwa.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiangalia mashine ya kukagua magari kwa njia ya umeme iliyokua inaonyeshwa na Mhandisi Yakubu Kibingo wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA. Katikati ni Meneja wa Karakana ya magari na mitambo mbalimbali ya Serikali, Julius Humbe. Masauni alifanya ziara katika ofisi hiyo iliyopo Keko, jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji nchini (NIT), Profesa Zakaria Mganilwa (katikati) alipokua anatoa historia ya chuo hicho pamoja na kozi mbalimbali zinazofundishwa katika chuo hicho, kilichopo Mabibo jijini Dar es Salaam. Masauni alifanya ziara chuoni hapo kwa lengo la kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini. Kulia ni Naibu Mkuu wa Chuo hicho kwa upande wa Taaluma Utafiti na Ushauri, Dk. Prosper Mgaya.
Mkuu wa Idara ya Teknolojia ya Usafirishaji wa Chuo cha Usafirishaji nchini (NIT), kilichopo Mabibo, jijini Dar es Salaam, Amon Mwasandube, akimuonyesha Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), jinsi gari
linavyokaguliwa linapokuja katika Kituo cha Ukaguzi wa Magari chuoni hapo. Masauni alifanya ziara chuoni hapo kwa lengo la kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Zakaria Mganilwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Na Felix Mwagara (MOHA)
MWENYEKITI wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema Baraza lake litakutana kujadili uwezekano wa Jeshi la Polisi, Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) pamoja na Chuo cha Usafirishaji (NIT) ziweze kuungana ili kufanya ukaguzi wa lazima wa magari kwa lengo la kuondoa ajali nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea ofisi za Temesa
na Chuo cha NIT, Masauni alisema ziara yake ilikua na mafanikio makubwa, hivyo anatarajia kukutana na Wajumbe wa Baraza lake katika vikao vyao na kuwasilisha uzoefu alioupata mara baada ya kuzitembelea Taasisi hizo za Serikali.
“Nimeshuhudia Temesa na NIT mambo ambayo sikuyatarajia, inaonyesha kwamba katika vita ya kuzuia ajali nchini hatutaanza sifuri, tunasehemu fulani ya kuanzia, tutaanza na utaratibu wenye mfumo mzuri ambao utaweza kutekelezwa ili kufikia malengo ya kuwa na utaratibu wa lazima wa ukaguzi wa magari yote ambayo yanatumika katika nchi yetu,” alisema Masauni na kuongeza;
“Lengo la mipango hiyo ni kuhakikisha tunakuwa na magari mazuri ambayo hayawezi kusababisha ajali,
hivyo nitawasilisha katika kikao hicho chha Baraza uzoefu huu nilioupata baada ya ziara hii ili nijadiliane na wajumbe wenzangu tuone jinsi tutakavyokubaliana kuhusiana na mafanikio niliyoyapata baada ya ziara hii.”
Post a Comment