"Jengo la Yanga kupigwa mnada"

                                                                   Jengo la Yanga lililopo Jangwani jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amefunguka na kuwapa pole watani wake wa jadi klabu ya Yanga kufuatia taarifa iliyotoka katika moja ya gazeti kuonyesha jengo lao litapigwa mnada Jumamosi ya wiki hii.
 Haji Manara ametoa pole hiyo kupitia ukurasa wake wa Instgram na kuwaombea watani wao wajadi kwa kusema hivi sasa hali yao si nzuri hivyo kama jengo hilo kitauzwa watakwenda kukaa wapi. 
"Mungu wangu,Jumosi hii jengo la Yanga linapigwa mnada, Wizara ya Ardhi waoneeni huruma kidogo wenzetu wana Swaumu kali, Daah!!sasa watahamia wapi? Shubamit" alimalizia Haji Manara 
Jengo la klabu ya Yanga jijini Dar es Salaam linatarajiwa kupigwa mnada Agosti 19 kwa amri ya Mahakama baada ya kudaiwa kodi ya ardhi zaidi ya milioni 300. 
Mbali na hilo klabu ya Simba na Yanga zote zipo visiwani Zanzibar zikijipanga kwa ajili ya mchezo wa ngao ya jamii unaowakutanisha watani hao katika uwanja wa Taifa siku ya Jumatano ya tarehe 23 Agosti 2017. ]
]chanzo; eatv.tv


No comments

Powered by Blogger.