Barabara ya Morocco – Mwenge kuwa na njia nane
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameishukuru Japan kwa kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi Jijini Dar es Salaam ikiwemo upanuzi wa barabara ya Mwenge – Morocco utakaoiwezesha barabara hiyo kuwa na zaidi ya njia nane.
Rais Magufuli alitoa shukrani hizo jana alipokutana na kufanya mazungumzo na aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Ichiro Aisawa ambapo ujenzi wa barabara ya TAZARA, ujenzi wa Daraja la Gerezani njia nne, na barabara ya Bendera tatu hadi Kamata.
Aidha Rais Magufuli alimuomba Mhe. Ichiro ambaye ni mwakilishi wa wabunge wa Japan wanaoshughulikia masuala ya Afrika kuwahamasisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Japan kuja kuwekeza hapa nchini na ameahidi kuwa Serikali itahakikisha uwekezaji wao unalindwa kama itakavyofanya kwa kampuni ya kutengeneza rangi ya Kansai Plascon ambayo awali ilijulikana kama Sadolin, na kampuni inayozalisha Betri za Panasonic hapa nchini, ili uwekezaji huo ulete manufaa hapa nchini.
Post a Comment