WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHITIMISHA ZIARA YA MKOA WA SONGWE


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  watumishi wa umma, viongozi wa dini na wananchi katika kikao cha majumuisho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya  Sunrise wilayani Mbozi Julai 24, 2017. Kulia ni mkewe Mary, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa na wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Songwe, Erasto Zambi. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).
 Baadhi ya watumishi wa umma, viongozi wa dini na wananchi wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao  katika kikao cha majumuisho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya  Sunrise wilayani Mbozi Julai 24, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea silaha za jadi kutoka kwa Chifu  Muleshwelwa Mzunda wa Mbozi ikiwa ni ishara ya kusimikwa kuwa Chief wa Songwe Julai 24, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika ziara ya mkoa wa Songwe . Kushoto kwake ni mkewe Mary na watatu kulia  ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kushoto kwake) wakiagana na viongozi wa Mkoa wa Songwe kabla ya kuondoka kwenye makazi ya Mkuu wa Mkoa huo kwenda kwenye uwanja wa ndege wa Songwae baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani humo Julai 24, 2017. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nanyara wilayani Mbozi ambao walikusanyika barabarani wakitaka asimame na kuzungumza nao . Alikuwa akitoka Vwawa kwenda Uwanja wa Ndege wa Songwe Julai 24, 2017.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments

Powered by Blogger.