SERIKALI YA TANZANIA YAPONGEZWA KWA KUWALINDA WATU WENYE UALBINO

 Serikali ya Tanzania imepongezwa kwahatua inazochukua kuwalinda watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino) jambo ambalo limepunguza matukio ya ukatili ambayo wanafanyiwa watu hao.
Hayo yamesemwa na mtaalam wa kujitegemea anayeshughulikia haki za watu wenye ualbino aliyeteuliwa na Baraza la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Haki za Binadamu, Ikponwosa Ero baada ya kufanya ziara ya siku 11 nchini kujione hali ilivyo kwa wtu wenye ualbino.
“Ninapongeza hatua zilizochukuliwa na Serikali na asasi za kirai ili kupunguza idad ya mashambulizi dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi ikiwa ni pamoja na kushughulikia vitendo vya kichawi pamoja na usajili wa waganga wa tiba za jadi,” alisema Ero.
Pamoja na pongezi hizo ambazo pia Ero aliitaka serikali kuongeza juhudi ili matukio ya kikatili ambayo wamekuwa wakifanyiwa watu wenye ulemevu wa ngozi (ualbino) yaishe kabisa.
Mtaalam wa kujitegemea anayeshughulikia haki za watu wenye ualbino aliyeteuliwa na Baraza la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Haki za Binadamu, Ikponwosa Ero akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku 11 za ziara yake nchini.

Pia Ero ameiomba serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waachane na mila potofu zinazowahusu watu wenye ualbino jambo ambalo litapunguza changamoto ambazo zinawakabili,

“Licha ya kuwa na dhamira nzuri ya ulinzi wa kuwahifadhi watoto wenye ulabino katika vituo vya shile kwa ajili ya ulinzi thabiti lakini bado kuna changamoto zinawakabili,

“Serikali inatakiwa kuendelea kuelimisha jamii na kuimarisha ulinzi kwa sababu baadhi ya jamii haitaki kuwakubali watu wenye ualbino,” alisema Ero.

No comments

Powered by Blogger.