RAIS WA BARCELONA ASEMA NEYMAR HATAONDOKA BARCELONA

Neymar hataondoka Barcelona licha ya Paris St-Germain kuwa tayari kutoa ada ya paundi milioni 195, rais wa klabu Josep Maria Bartomeu amesema.

Mshambuliaji huyo raia wa Brazili, ametia saini mkataba mpya wa miaka mitano hadi 2021 Oktoba, huku ada ya kumg'oa ikiongezeka kila mwaka.

Timu za Manchester United na Chelsea nazo zilikuwa zinamuwania Neymar ila ziliamua kujitoa baada ya kusikia dau la Paris Saint-Germain la paundi milioni 195.

No comments

Powered by Blogger.