OKWI AANZA MAZOEZI SIMBA, KILA KITU SHWARI
Baada ya maelezo na tetesi nyingi, hatimaye mshambuliaji Emmanuel Okwi ametua na kuanza mazoezi katika kikosi cha Simba.
Okwi ametua kikosini hapo akitokea Uganda ambapo alikuwa katika majukumu ya timu ya taifa ya Uganda, jana Ijumaa alisafiri na kutua Afrika Kusini kujiunga na kambi ya timu hiyo iliyopo nchini humo ambapo ameanza mazoezi leo Jumamosi.
Kutua kwa Okwi kunamaanisha kila kitu kimeenda vizuri kwa kuwa uongozi wa Simba uliweka wazi kuwa utakapoelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kambi mchezaji huyo naye ataelekea huko kuanza mazoezi kisha watarejea naye pamoja kwa jili ya mchezo wa Simba Dar.
Post a Comment