KAMUSOKO YUPO DAR, MKATABA WAKE NA YANGA UNAMALIZIKA, HUU NDIYO MWELEKEO WAKE

Kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko amesharejea jijini Dar es Salaam akitokea kwenye mapumziko na yupo kwenye hatua za mwisho kuongeza mkataba mpya wa kuichezea Yanga.
Kamusoko anatarajiwa kumaliza mkataba wa kuichezea Yanga mwezi huu baada ya kuichezea kwa mafanikio tangu alipotua akitokea FC Platinum ya Zimbabwe, amefanikiwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara mbili mfululizo, Ngao ya Jamii na Kombe la FA.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa mchezaji huyo anaweza kusaini mkataba huo muda wowote kuanzai leo Jumamosi.

No comments

Powered by Blogger.