AY NDOA SOON...AMVISHA PETE MCHUMBA WAKE

                                                                       Hakika ni furaha.
  Rapper nguli asiyechuja tangu kitambo hicho kutoka Bongo Fleva, Ambwene Allen Yessayah maarufu kama A.Y ama ‘Mzee wa Ankara’, ‘Mzee wa Commercial’ amedhihirisha kuwa kwa sasa yuko tayari kuachana na ukapela baada ya kumvalisha pete ya uchumba mpenzi wake wa muda mrefu, Remy.
                                            A.Y akimvisha pete mchumba wake, Remy. 
Tukio hilo lilifanyika jana Alhamisi ambapo A.Y alimvalisha pete mrembo huyo ambaye ni raia wa Rwanda na amekuwa naye katika mahusiano tangu mwaka 2008.
                                                                   Pete imo kidoleni.
  Kwa mara ya kwanza AY alimtambulisha mpenzi wake huyo Desemba mwaka jana wakati wa siku ya kuzaliwa ‘birthday’ ya mrembo huyo.
A.Y, Remy, na marafiki wa karibu wakipiga picha ya pamoja baada ya tukio la kuvalishwa pete.
  Sherehe hiyo ilihudhuriwa na watu wa karibu na wawili hao. Kwa kitendo hicho tunatarajia kuiona ndoa ya A.Y na mpenzi wake huyo siku chache zijazo akiwafuata mastaa wengine kama MwanaFA, R.O.M.A, Prof, Jay ambao wamefunga ndoa na wana-enjoy maisha ya familia.

No comments

Powered by Blogger.