MICHUANO YA KOMBE LA MABARA KUANZA LEO JUMAMOSI, RONALDO YUPO

Michuano ya Kombe la Mabara inatarajiwa kuanza leo Jumamosi nchini Urusi ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya kufanyika kwa fainali za Kombe la Dunia ikishirikisha mataifa nane.
Kuelekea Michuano hiyo Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limewataka waamuzi watakochezesha kusimamisha mchezo au kuuvunja endapo Mashabiki watakashifu na kutoa lugha za kibaguzi viwanjani wakati wa Mechi.
Urusi ambao ndiyo wenyeji wa fainali za kombe la Dunia za Mwaka 2018, hawana sifa nzuri ya kutenda haki uwanjani na mara nyingi kumekuwa tabia za kibaguzi, na FIFA imedai kuwa itaweka waangalizi wa mambo ya kibaguzi viwanjani.
Wenyeji Urusi wataanza michuano hiyo kwa kuikabili New Zealand kundi A, Jumapili Ureno watachuana na Mexico huku Cameroon ikimenyana Kundi B.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo anatarajiwa kuiongoza timu ya taifa ya Ureno katika michuano hiyo.

No comments

Powered by Blogger.