Breaking News: Mdee, Bulaya Wasimamishwa Kuhudhuria Bunge Hadi Mwaka 2018
DODOMA: Mbunge wa Kawe, Halima
Mdee na Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya wote wa CHADEMA wameadhibiwa
kwa kusimamishwa na Bunge kuhudhuria vikao vyote vilivyosalia vya
mkutano wa 7 wa Bunge la Bajeti linaloendelea hivi sasa mjini hapa, pia
hawatohudhuria mkutano wa 8 na wa 9 kwa utovu wa nidhamu.
Aidha Bunge limeamua kuwa, wabunge hao watarudi kuhudhuria vikao kuanzia kwenye Bunge la Bajeti la mwaka ujao (2018).
Tukio hilo limeibuka kufuatia vurugu zilizoibuka Ijumaa iliyopita baada ya Mbunge wa Mvumi, Livingstone Lusinde kudai kwamba wapinzani bungeni humo wanatetea wezi wa mchanga wa dhahabu, hali iliyosababisha Mbunge wa Kibamba, John Mnyika kuibuka na kubishana. Mbunge mwingine ambaye hakujulikana jina lake aliwasha maiki na kumuita Mnyika mwizi, Mnyika alikitaka kiti cha Spika kimuamuru mbunge huyo kufuta kauli yake lakini spika alisema hakumsikia aliyesema maneno hayo.
Baada ya mabishano kati ya Spika na Mnyika, spika aliamuru Mnyika atolewe nje na polisi wa Bunge, hali iliyosababisha Halima Mdee na Ester Bulaya, waiingilie kati kuwazuia askari hao kumtoa nje. Jambo hilo lilisababisha tafrani licha ya Mnyika kutolewa nje huku wabunge wa upinzani wakitoka nje.
Spika alitangaza kumsimamisha Mnyika asihudhurie vikao vya bunge kwa wiki moja huku akisema Ester Bulaya na Halima Mdee wataandikiwa barua ili wakahojiwe na Kamati ya Haki na Maadili ya Bunge ambapo leo wameadhibiwa wasihudhurie vikao vya bunge kama ilivyoelezwa hapo mwanzo.

Post a Comment