VIDEO: Rais Magufuli Amuapisha Simon Sirro Kuwa IGP Mpya

 Rais Magufuli akimvua cheo cha Kamishna wa Polisi, Simon Sirro na kumvalisha cheo cha Inspekta Generali wa Jeshi la Polisi Tanzania. 

IKULU: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumatatu Mei, 29, 2017 amemuapisha rasmi aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) akichukua nafasi ya Ernest Mangu.Katika hafla hiyo ya kuapishwa kwa IGP Sirro viongozi mbalimbali wa serikali wamedhudhuria ambao ni pamoja na Makamu wa Rais, Bi. Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. John Kijazi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba na aliyekuwa IGP, Ernest Mangu. Zoezi la kuapishwa, lilienda sambamba na kula kiapo cha maadili ya utumishi wa umma kisha likafuatia zoezi la upigaji wa picha za pamoja. kabla ya kuteuliwa kuwa IGP, Sirro alikuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
 Rais Magufuli akimvua cheo cha Kamishna wa Polisi, Simon Sirro na kumvalisha cheo cha Inspekta Generali wa Jeshi la Polisi Tanzania.
 Rais Magufuli akimvua cheo cha Kamishna wa Polisi, Simon Sirro na kumvalisha cheo cha Inspekta Generali wa Jeshi la Polisi Tanzania.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi Simon Sirro akila kiapo mbele ya Rais kuwa Ispekta Generali wa Jeshi la Polisi Nchini.
 Inspekta Jenerali wa Polisi Nchini, Simon Sirro akisaini hati ya kiapo cha maadili ya utumishi wa umma mara baada ya kuapishwa.

No comments

Powered by Blogger.