Steven Wasira Arudi Kortini Kumng’ang’ania Bulaya........Rufaa Yake Itasikilizwa Kesho
Mahakama ya Rufaa Tanzania imepanga kusikiliza rufaa ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Bunda kesho.
Mahakama
hiyo ilitoa uamuzi huo jana katika rufaa iliyokatwa na wapigakura wanne
wa jimbo hilo baada jopo la majaji watatu kukwama kuanza kusikiliza kwa
sababu ya makosa yaliyofanyika kwa vile Wakili wa Mbunge wa Jimbo
hilo, Ester Bulaya, Tundu Lissu hakuipata notisi ya kuitwa mahakamani.
Jopo
la majaji linaloongozwa na Jaji Mbarouk Mbarouk liliahirisha
usikilizwaji huo hadi kesho na kuamuru makosa hayo yasirudiwe tena kwa
kuwa yamewapotezea muda na wana mambo mengi ya kufanya.
Warufani
wanawakilishwa na mawakili Yassin Member na Constantine Mutalemwa huku
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akiwakilishwa na Mawakili wa
serikali, Obadia Kamea na Angela Msagala.
Wakili
wa mjibu rufani wa kwanza wa Bulaya, Lissu hakuwapo mahakamani hivyo
mawakili wa wakata rufaa waliomba kesi iahirishwe kwa muda mfupi
kutokana na umuhimu wake.
Jopo
hilo, Jaji Mbarouk, Augustino Mwarija na Rehema Mkuye, lilikubaliana na
ombi hilo, hivyo kuamua kuahirisha usikilizwaji huo hadi kesho.
“Inasikitisha,
haipendezi mnaopeleka notisi muwe makini kwa sababu mnatupotezea muda
wakati tuna mambo mengi ya kufanya, hili kosa lisijirudie tena, sisi
tulikuwa tayari kusikiliza na tulipanga kesi moja tu,” alisema Jaji Mbarouk.
Wakata
rufaa katika kesi hiyo ya uchaguzi Jimbo la Bunda ni Magambo Masato,
Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagila ambao walikata rufani
dhidi ya Bulaya, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali (AG).
Wakili
Mutalemwa alitaja sababu za kukata rufani kwamba uchaguzi haukuwa huru
na haki kutokana na ukiukwaji wa wazi wa sheria za uchaguzi na kanuni.
Alidai
tafsiri isiyo sahihi ya kanuni za uendeshaji kesi za uchaguzi kuhusiana
na viapo na kutofuatwa kwa taratibu za uchaguzi kwa kutomtaarifu
mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mahali na tarehe ya kujumuisha
kura na taarifa ya mwisho ya matokeo kuwa na idadi kubwa ya
waliojiandikisha kupiga kura tofauti na Tume ya Uchaguzi ya Taifa.
Post a Comment