MABADILIKO AZAM FC, SAAD KAWEMBA APIGWA CHINI, BOSI MPYA WA AZAM FC NI HUYU HAPA…

Katika kile ambacho kinaonekana ni kuitengeneza klabu kuwa kwenye mwelekeo sahihi, taarifa ni kuwa Klabu ya Azam imefanya mabadiliko ya kiungozi ambapo Saad Kawemba amewekwa pembeni.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa Kawemba ambaye alikuwa Mtendaji Mkuu wa Klabu (CEO) sasa amewekwa pembeni baadaya mkataba wake kumalizika na kisha nafasi hiyo imeenda kwa Abdul Mohamed ambaye alikuwa meneja wa timu.
Ikumbukwe kuwa Azam FC ambao ni mabingwa watetzi wa Kombe la Kagame ilimteua Abdul Mohamed kuwa Meneja Mkuu wa timu hiyo, Oktoba Mosi, mwaka jana akitokea Uingereza alipokuwa akisoma na kufanya kazi pia katika Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) nchini humo.
Kitaaluma Mohamed ni mwandishi wa habari ambaye amewahi kufanya kazi katika makampuni ya IPP Media na Clouds Media, pia ni msomi aliyesomea masuala ya Uhasibu na Fedha.

No comments

Powered by Blogger.