MENEJA WA SIDO MKOA WA MTWARA AZINDUA RASMI MAFUNZO YA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI CHINI YA TAASISI YA MANJANO FOUNDATION
Akieleza zaidi amesema “Shekha Nasser ni moja ya wawekezaji wa ndani ambao wanapaswa kuungwa mkono kwani ameamua kuwekeza na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutumia bidhaa za LuvTouch ambazo zimesajiliwa hapa hapa nchini kuwawezesha wanawake kupata elimu ya ujasiriamali ili waweze kujiajiri na kujiongezea kipato kupitia bidhaa hizo”
Baada ya kuhitimu mafunzo haya washiriki hao wataunganishwa na Taasisi za kifedha ili kuweza kupata mikopo ya kupata mitaji ya kuanzisha bishara
Mwezeshaji Kutoka Taasisi ya Manjano Foundation Bi Ester Lukindo Akizungumza Machache wakati wa Uzinduzi Huo . Bi Ester Lukindo aliyesoma hotuba kwa niaba ya afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions na Muasisi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama “Shekha Nasser alisema kuwa "wasichana ambao wanapata mafunzo kutoka taasisi hiyo wanaweza kujikwamua na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa kuchangamkia fursa zilizopo kwenye tasnia ya Urembo."
Post a Comment