Basata Wasema Wimbo wa Nay wa Mitego Umejaa Matusi
Katibu
Mkuu wa Basata, Godfrey Mngereza ameeleza kuwa Baraza liliusikiliza
wimbo huo na kubaini kuwa ni wimbo usiofaa kwa jamii na zaidi unachochea
vurugu.
“Ule
wimbo tumeusikiliza, kama Baraza tunasema ule wimbo hauna maadili, ni
wimbo ambao una matusi, ni wimbo ambao unachochea vurugu, ni wimbo ambao
haufai kwa jamii,” alisema.
Aliongeza kuwa vyombo vyote vya habari ambavyo vitaucheza wimbo huo vitakumbwa na mkono wa sheria kutoka kwa vyombo husika.
Nay
wa Mitego alikamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro majira ya saa
nane usiku, na lifikishwa Dar es Salaam anakoshikiliwa kwa mahojiano na
Jeshi la Polisi.
Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, Kamanda Ulrich
Matei alithibitisha kukamatwa kwa msanii huyo usiku wa kuamkia jana.
Kupitia
ukurasa wake wa Instagram, wakili Peter Kibatala amesema kuwa
atasimamia kesi dhidi ya msanii huyo na kwamba tayari ameshamjulia hali
katika kituo cha kati jijini Dar es Salaam.
Post a Comment