JERMAIN DEFOE ARUDI KIMATAIFA KWA KUTUPIA GOLI WAVUNI

Uingereza imepata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Lithuania katika mchezo wa kuwania kufuzu kutinga michuano ya kombe la Dunia.

Katika mchezo huo Jermain Defoe alifunga goli lake la kwanza tangu arejee kimataifa baada ya miaka minne naye Jamie Vardy akafunga goli la pili dakika sita tangu aingie dimbani.

Uingereza inaendelea kuwa na rekodi ya kutofungwa katika kundi F, ingawa kikosi hicho cha Gareth Southgate hakikucheza mchezo mzuri hapo jana.
            Mshambuliaji Jermain Defoe akiifungia Uingereza goli la kwanza
              Jamie Vardy akiifungia Uingereza goli la pili katika mchezo huo

No comments

Powered by Blogger.