Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amekanusha tuhuma za kuhusika na
dawa za kulevya ikiwa ni siku chache baada ya kutajwa na mkuu wa mkoa wa
Dar es Salaam Paul Makonda katika orodha ya watu 65 wanadaiwa kuhusika
na dawa za kulevya.
Akizungumza na wanahabari leo Mjini
Dodoma Mbowe amesema hajawahi kujihusisha kwa kufanya biashara wala
kutumia madawa ya kulevya wakati wote katika maisha yake.
Pia Mbowe amesema kuwa vita hiyo
imechelewa sana kuanza kwani ilipaswa kuanza miaka mingi iliyopia, kwa
kuwa imekuwa ikididimiza mandeleo ya Taifa.
Mbowe amesema kuwa CHADEMA inaunga mkono
vita dhidi ya dawa za kulevya na iko tayari kuungana na yeyote
atakayeiendesha bila kujali, lakini haiko tayari kuunga mkono vita yenye
ila ndani yake.
Post a Comment