CAMEROON MABINGWA WA MICHUANO YA AFCON 2017

Cameroon imetokea nyuma ikiwa imefungwa goli moja na Misri na kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 na kutwaa ubingwa mara tano wa Kombe la Mataifa ya Afrika.

Mchezaji aliyetokea benchi Vincent Aboubakar alifunga goli la ushindi dakika mbili kabla ya mpira kumalizika akiupaisha mpira juu ya beki Ali Gabr na kutikisa nyavu.

Alikuwa Nicolas Nkoulou aliyeisawazishia goli Cameroon, baada ya kuruka juu na kufunga kwa mpira wa kichwa.

Misri ilikuwa ya kwanza kupata goli lililofungwa na Mohamed Elneny katika dakika ya 22 kwa shuti safi la karibu ya goli.
                      Mohamed Elneny akifunga goli la kwanza katika mchezo huo
            Nicolas Nkoulou akiruka juu na kuupiga mpira kwa kichwa na kusawazisha goli
       Vincent Aboubakar akijipinda na kuachia shuti lililojaa wavuni na kuipa ushindi Cameroon

No comments

Powered by Blogger.