Exclusive News: Charles Boniface Mkwasa Ateuliwa Kuwa Katibu Mkuu wa Yanga

 DAR ES SALAAM: ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Timu ta Taifa Tanzania  ‘Taifa Stars’ Charles Boniface Mkwasa ameteuliwa na kutangazwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Klabu ya Yanga kuchukua nafasi ya Baraka Deusdedit ambaye anashushwa na kuwa mhasibu wa klabu hiyo.
 Mkwasa ambaye aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Yanga na baadaye Kocha Mkuu wa Taifa Stars, huenda ametangazwa rasmi leo Januari 31 kuchukua nafasi hiyo.Aidha imeelezwa kuwa, Charles Boniface Mkwasa  ataanza kazi rasmi kesho katika nafasi yake ya Katibu Mkuu mpya Yanga.Mkwasa anakuwa mchezaji mwingine wa Yanga baada ya Lawrance Mwalusako kushika wadhifa huo wa utendaji Wakati akiwa mchezaji, alikuwa kiungo nyota wa Yanga na Timu ya Taifa Stars.Yanga inatarajia kumtangaza leo na Mkwasa atachukua nafasi ya Baraka Deusdedit aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo ambaye imeelezwa anashushwa na kuwa bwana fedha.Awali ilionekana, huenda Baraka angechukua nafasi hiyo na kuwa katibu kamili wa Yanga, hata hivyo ikaonekana hakuwa amefanya utendaji katika kiwango kilicho sahihi kama ambavyo uongozi wa Yanga ulitarajia.

No comments

Powered by Blogger.