Waziri Kigwangalla ajibu kwanini serikali ya China isichangie gharama ya matibabu ya waathirika wa ajali za bodaboda

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Hamisi Kigwangalla amesema vyombo hivyo vinavyoingia nchini kuna mamlaka mbalimbali zinazosimamia uingiaji wake, mamlaka hizi ni pamoja na zile za udhibiti ubora yaani TBS na mamlaka ya mapato TRA ambapo hulipiwa ushuru kabla havijaingia sokoni.Amezungumza hayo Jumanne hii Bungeni mjini Dodoma, Dkt Kigwangalla wakati akijibu swali, lililohoji “Kwanini Serikali ya Jamhuri China isichangie gharama za matibabu kwa wananchi wanaopata ajali za bodaboda?”
“Muheshimiwa spika ni kweli kumekuwa na ongezeko kubwa la ajali za bodaboda ambazo zinaongeza gharama za matibabu,ongezeko la ajali hizi limekuwa likichangiwa na sababu mbalimbali ikiwa vifaa hivi kutofanyiwa matengenezo mara kwa mara,madereva kukosa umakini,ulevi,uzoefu na miundombinu chakavu,”amesema Kigwangalla.
“Muheshimiwa spika vyombo hivi vinavyoingia nchini kuna mamlaka mbalimbali zinazosimamia uingiaji wake mamlaka hizi ni pamoja na zile za udhibiti ubora yaani TBS na mamlaka ya mapato TRA ambapo hulipiwa ushuru kabla havijaingia sokoni, Aidha kabla mtumiaji hajaanza kutumia kwa biashara ina mlazimu kukata leseni ambayo pia hukusanywa na serikali,”ameongeza.
“Ni vyema kufahamu pikipiki zinazoingia nchini zinatoka nchi mbalimbali si china peke yake,suala la ajali za barabarani halikubaliki na halizuiliki ninaomba wote tukemee vitendo vya uendeshaji mbaya wa bodabodaili kulinda uhai wa wananchi wetu”.
Aidha ameliomba jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kuendelea kulisimamia suala hili ili kupunguza ajali za barabarani zinazoweza kuepukika.
BY: EMMY MWAIPOPO

No comments

Powered by Blogger.