SMZ Yakanusha Taarifa za Kifo cha Balozi Omar Ramadhan Mapuri
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inapenda kukanusha taarifa kutoka
kwenye baadhi ya Mitandao ya Kijamii ikidai kwamba, Kamishna wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar, Balozi Omar Ramadhan Mapuri (pichani) amefariki
dunia.
Taarifa rasmi ya serikali ni kwamba taarifa hizo ni za uongo na hazina hata chembe ya ukweli, Kamishna Balozi Mapuri yupo hai na afya yake iko vizuri.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi alipokwenda kumjulia hali Kamishna wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mh. Omar Ramadhan Mapuri katika Hospitali ya
Rufaa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed akimpa pole Mhe.
Mapuri aliyekuwa Hospitali ya Muhimbili akipatiwa matibabu.
Imetolewa na :
Dk. Juma Mohammed Salum
Kny Mkurugenzi
Idara ya Habari MAELEZO
Zanzibar
Taarifa rasmi ya serikali ni kwamba taarifa hizo ni za uongo na hazina hata chembe ya ukweli, Kamishna Balozi Mapuri yupo hai na afya yake iko vizuri.
Mheshimiwa Balozi Omar Ramadhan Mapuri
ambaye kwa sasa ni Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar alilazwa katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipata matibabu na baada ya
kupata huduma kutoka kwa madaktari, Mheshimiwa Balozi Mapuri aliruhusiwa
kurejea nyumbani siku ya Jumamosi Novemba 12 baada ya afya yake
kuimarika.
Serikali imesikitishwa na taarifa za uvumi
na uzushi uliosambazwa jana na leo kwenye mitandao ya kijamii, taarifa
hizi siyo za kweli na tunawaomba wananchi wazipuuze.
Aidha, Serikali inapenda kuvionya vyombo vya habari na Mitandao ya
Kijamii kuacha kusambaza taarifa za uongo kuhusu viongozi wa Serikali. Imetolewa na :
Dk. Juma Mohammed Salum
Kny Mkurugenzi
Idara ya Habari MAELEZO
Zanzibar
Post a Comment