Moto Wateketeza Godauni la Matairi Mikocheni Dar
DAR ES SALAAM: Moto mkubwa ambao mpaka sasa bado unawaka umeteketeza godauni la kuhifadhia matairi la Kampuni ya 7 General linalomilikiwa na Wahindi lililopo karibu na Chuo Kikuu cha Tumaini eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Tovuti hii imefanikiwa kufanya mahojiano
na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo aitwaye Shaban Salum ambaye
ameeleza kuwa chanzo cha moto huo mkubwa na wa aina yake ambao
unaonekana ni vigumu kuuzima ni shoti ya umeme.
Timu ya Kikosi cha Zimamoto imewahi
kufika eneo la tukio ikiwa na magari takribani matano na kufanya juhudi
za kuuzima moto huo lakini hawajafanikiwa. Mpaka sasa maji yameisha na
magari mengine yamefuata maji mengine kwa ajili ya kuendelea na zoezi la
uzimaji.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi
wa Kinondoni, Suzan Kaganda yupo eneo la tukio ili kuona jinsi ya
kuongeza nguvu katika zoezi la uokoaji mali pamoja na kuzima moto huo.
PICHA ZOTE NA HILALY DAUD / GPL
Post a Comment