Milionea Anayelipa Bilioni 20 kwa Ajili ya Plate Number ya Gari
Balwinder Sahni ambaye anafanya biashara zake nchini Dubai hutumia gharama hiyo kulipia ili aendelee kuimiliki plate number ya moja ya magari yake 6 aina ya Rolls Royce.
Balwinder Sahni, ambaye anamiliki mali nyingi mjini humo ameiambia CNN kuwa, anaipenda sana plate number yake hiyokwani inamsaidia kumtangaza hivyo kumrahisishia na kumuongezea watu wengi ambao humtafuta ili kufanya naye biashara.
Pia husikitishwa na watu wanaomshutumu kuwa anatumia pesa zake vibaya.
“Ni vigumu, watu wanasema bila kufahamu mimi ni nani. Mimi ni mtu wa kawaida tu.” Sahni aliiambia CNN Money.
Post a Comment