MANNY PACQUIAO AREJEA ULINGONI NA KUTWAA MKANDA WA WBO

Bondia Manny Pacquiao amerejea ulingoni na kupata ushindi wa majaji wote dhidi ya bingwa wa mkanda wa WBO, Jessie Vargas, na kutwaa mkanda huo wa uzito wa welterweight Jijini Las Vegas.



Bingwa huyo wa zamani wa dunia Pacquiao, 37, alitangaza kujiuzulu masumbwi baada ya kumpiga Timothy Bradley mwezi Aprili.



Katika mchezo wa jana usiky matokeo ya majaji wote watatu yalikuwa ni pointi 114-113, 118-109 na 118-109 yakionyesha Mfilipino Pacquiao ndiye mshindi kwenye pambano hilo.
     Bondia Manny Pacquiao akimsukumizia konde la kulia Jessie Vargas
             Jassie Vargas akimrushia ngumi ya tumboni Manny Pacquiao
      Bingwa wa zamani wa dunia Floyd Mayweather Jr akifuatilia pambano hilo

No comments

Powered by Blogger.