Mwanadada kutoka Nigeria, Yemi Alade akizikonga nyoyo za mashabiki
waliohudhuria tamasha la Fiesta 2016 Imoooo katika Viwanja vya Leaders
Club jijini Dar es Salaam leo Novemba 5, 2016.
Mwanamuziki kutoka Nigeria, Tekno Miles akilishambulia jukwaa la Fiesta 2016.
Mashabiki waliofurika kwenye shoo ya Fiesta 2016 hapo jana ndani ya Viwanja vya Leaders Club
. Tekno na vijana wake wakifanya yao.
Tekno akirusha viatu vyake kwa mashabiki.
Ali Kiba “King Kiba” akiwapa raha mashabiki wake waliofurika katika Viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya Fiesta 2016.
King Kiba akiimba sambamba na King of the best melodies, Christian Bella
. King Kiba akizidi kuwapa raha mashabiki.
Baraka Da Prince akikatika sambamba na madansa wakati akiimba wimbo aliomshirikisha Ali Kiba.
Mwana Hip hop, Roma Mkatoliki akishusha mistari juu ya jukwaa la Fiesta 2016.
Roma Mkatoliki na Stamina wakiwa stejini na mavazi yao ya mabondia.
Chid Benz akifanya yake.
Mr Blue akiwapagawisha mashabiki waliofurika katika hitimisho la msimu wa Fiesta 2016.
Mwanamuziki Chegge Chigunda na madansa wake wakionyesha umahiri wao stejini.
Baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media ambao ni waandaaji wa Fiesta wakiwa stejini.
Mwanamuziki Ben Pol akiwaburudisha mashabiki.
Mtangazaji wa Clouds FM, Adam Mchomvu akisema na mashabiki
Dogo Janja akikisanua stejini.
Mzee wa Too Much, Darasa akiwapa shangwe wapenda burudani.
Mwanamuziki TID a.k.a Mnyama a.ka. Kigoo akifanya yake kwa steji.
King of the best melodies, Christian Bella akiwapa raha Wana Dar es Salaam.
Mwanamuziki Raymond “Rayvan” kutoka WCB akilishambulia jukwaa la Fiesta 2016 Imooo.
Post a Comment