Nyuma ya Pazia Diamond Kumfunika Kiba kwa ‘Yai’
NA ANDREW CARLOS, RISASI JUMAMOSI:
MWISHONI mwa wiki iliyopita,
gumzo kubwa kunako tasnia ya burudani Bongo ilikuwa juu ya hafla ya
utoaji Tuzo za MTV Afrika (MAMA) ambapo wawakilishi kutoka Bongo,
Vanessa Mdee ‘Vee Money’, Navy Kenzo, Yamoto Band, Diamond, Raymond na
Ali Kiba ‘King Kiba’ walitoka kapa.
Diamond Platinums
Mengi yameongelewa kuhusiana na tuzo
hizo kuonekana kama zilitolewa kwa upendeleo (Sauz na Nigeria) huku
chache zikitolewa kwa nchi tofauti za Afrika.
Ukiachilia mbali wawakilishi wetu
kuambulia patupu, mapema kabla ya kuanza kwa hafla hiyo, King Kiba
pamoja na Sauti Sol kutoka Kenya walialikwa kwenye mahojiano juu ya
muziki wao. Kiba alionekana mtu wa kutojiamini ambapo alikuwa akirudia
neno ‘you know’ mara kwa mara.
Mbali na hiyo yakaja mahojiano ‘red
carpet’ dakika chache kabla hafla hiyo haijaanza, napo Kiba alionekana
kujiumauma huku msanii mwenzake Diamond akionekana kumfunika kwa kutema
‘yai’ (Kiingereza) lililokomaa.
Diamond na Kanye West
Japokuwa yai bovu la Kiba liligeuka
gumzo kubwa mitandaoni ni ukweli ulio wazi kuwa Diamond wa zama zile si
Diamond huyu, Kiba wa kipindi kile anaweza kuwa Kiba huyuhuyu.
Namaanisha kwamba, Diamond alijipanga kuwa wa kimataifa lakini Kiba
hakujipanga zaidi ya kuonekana kama mtu aliyelala na kuamshwa ghafla na
nguvu za mashabiki.
Katika makala haya, yapo mambo yanayoonesha wazi vitu vilivyochangia Diamond kumfunika Kiba katika kutema yai.
Diamond na David.
Kujichanganya
Tangu Diamond ameanza muziki, amekuwa ni
mtu wa kuangalia mbele. Kujitoa ufahamu na kujichanganya mbele za watu
wenye mafanikio kumemfanya kufikia hapa alipo.
Ikumbukwe kuwa Kiba ndiye aliyeanza
kujulikana kimuziki kisha Diamond akafuata lakini alivyofuata
hakusimama, alipiga hatua kuanzia alipopata shavu la kuwa karibu na Bob
Junior (Sharobaro Records), Prof. Jay, AY, Davido (Nigeria) na sasa
Ne-Yo (Marekani).
Diamond na Ne-Yo
Kila ngazi aliyokuwa akipitia
alihakikisha anajiamini kwanza pasipo kuogopa, kitendo cha kukutana na
Davido katika Tamasha la Fiesta, 2013 kilimuonesha ukomavu wa kujua
kutema yai ambapo alitimba Nigeria na kutema yai na wengi wakiwemo
Iyanya, KCEE, Bracket, Tiwa Savage, Korede Bello, P-Square na sasa
anatema na Ne-Yo bila kujiumauma.
Upande wa Kiba, kwa muda mrefu amekuwa
si mtu wa kujichanganya na wenzake wa kimataifa, ukiangalia katika kazi
za nje ya nchi alizofanya ni wazi utazungumzia ya zamani (One8)
aliyofanya na R. Kelly na baadhi ya wasanii wa Afrika mwaka 2010 na hadi
leo hakuna chochote.
Zari na Diamond
Mastaa aliotoka nao kimapenzi
Siri nyingine ya Diamond kumfunika Kiba
kwa yai inatokana na mastaa aliotoka nao kimapenzi ambao ni Wema, Penny,
Jokate na sasa Zari.
Diamond alipoanzisha uhusiano na Wema
hakuwa akijua kutema yai kiufasaha na alishawahi kukiri kufundishwa na
Wema. Alipomwagana na Wema, alimpata Mtangazaji Penny ambaye naye kwenye
yai yupo fiti jambo lililomfanya kukuza yai lake.
Baada ya kutemana na Penny, akaangukia
kwenye penzi la Jokate ambaye naye kwenye yai yupo fiti, akaendelea
kujipiga msasa japo kwa kujiumauma. Hakudumu sana na Jokate akarudi kwa
Wema kisha akaangukia kwa mrembo kutoka Uganda, Zari ambaye amezaa naye
mtoto mmoja hadi sasa.
Lugha kuu ya Zari ni kutema yai kuliko
kuzungumza Kiswahili na hili limemfanya Diamond kukomaa zaidi na
kujiamini pale anapoulizwa kitu na mtu anayejua yai.
Ukija kwa Kiba napo ukiondoa uhusiano
wake na Jokate ambao si wa uhakika kivile, anadaiwa kuzaa na wanawake
tofauti ambao kwao yai limepita kushoto hivyo kumfanya asiwe mkali
katika kulitema.
Malengo
Diamond tangu aanze kutoka kimuziki
alijua siku moja atakuja kuwa wa kimataifa, akaanza kujiandaa mapema kwa
maana ya kujiweka kistaa kuanzia muonekano hadi kwenye kutema yai.
Licha ya kupata shavu la kufundishwa na
watu aliokuwa nao katika uhusiano, Diamond pia ametumia fedha kutafuta
walimu wa kumnoa ambapo hadi sasa katika lebo yake ya WCB wasanii wake
wengi wamenolewa.
Ukija kwa Kiba japo ni msanii mkongwe,
inaonekana hakuwa na malengo ya kufika mbali zaidi. Alitamba miaka ya
mwanzoni mwa 2000 lakini akapotea, nguvu za mashabiki zikamrudisha tena
baada ya kuanzisha Kampeni ya ‘Bring Back Our Mc’. Alivyorudi hakuwa
amejiandaa kimataifa bali kuonesha uwepo wake na kipaji chake.
Ushauri
Kiba ni miongoni mwa mastaa wakubwa
nchini, ana kipaji cha hali ya juu na ndiyo maana lebo kubwa duniani
(Sony) imemuona na kumsainisha. Kinacho-muangusha ni kutoji-amini nafasi
aliyonayo (ustaa) kama anaweza pamoja na kukubali kujifunza kila siku,
kama yai linaonekana kuwa gumu kidogo kwake zipo njia za ‘kusolve’ na
akapigwa msasa akawa sawa.
Post a Comment