Mwigulu Nchemba Afafanua kuhusu tuhuma za kughushi vyeti vya kitaaluma na kutumia jina la mtu mwingine.
Wakati
Serikali ikitangaza msako kwa watu walioghushi vyeti na kutumia majina
ya watu wengine, Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi, Mwigilu Nchemba,
ameibuka na kutoa ufafanuzi wa utata wa majina yake.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuibuka kwa mjadala wa usahihi wa majina yake pamoja na kuhusishwa kughushi vyeti ya elimu.
Katika
andiko lake aliloliweka jana katika mitandao ya kijamii ambalo baadaye
lilithibitishwa na mmoja wa wasaidizi wake, Mwigulu alisema watu
wanaoandika historia yake hawamjui kwani uhalisia alikuwa akiitwa Lameck
Madelu Mkumbo, sasa Lameck si jina la Kinyiramba na Madelu si jina
halisi la baba yake bali la utani.
“Ni
vema kuweka rekodi sawa, kwanza anasema (aliyeandika) nilikuwa naitwa
Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja Lameck sio jina la kinyiramba, na Madelu
sio jina halisi la baba bali ni utani kuwa ana ndevu nyingi, yaani ni
mandevu. Ndiyo maana hata kwenye ubunge nililiongeza tu kama a.k.a ili
watu, hasa wazee wanifahamu, hili haliko kwenye vyeti.
“Hili
la Lameck siyo jina la Kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea
zahanati iliyopo Kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo, lakini ni
nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck.
“Mimi
nilipelekwa hospitali nikiitwa Mugulo na jina la ukoo kwa watoto wote
wa kiume ni Shumbi, ambalo hata hivyo wanatumia wazee tu, wanaojua
Kinyiramba hilo ndio jina la Kinyiramba,” alisema Mwigulu na kuongeza:
“Mama
yangu aliulizwa jina akanitaja kwa muuguzi (nesi) akamwambia mama
unamwitaje jina hilo hakuna lingine, mama akamwambia hakuna labda mtaje
wewe, basi jamaa akajitaja,” alisema.
Alisema
suala hilo ni jambo la kawadai hasa kwa kijijini kwani familia inakuwa
na watoto wengi hadi majina inakuwa si jambo la kujali.
“Hata
pale kijijini kuna wengine waliotajwa majina ya waganga wa kienyeji
wazee walikopewa dawa, majina ya manesi, matabibu kama mimi, majina ya
walimu,” alisema.
Akizungumzia
maisha yake ya elimu, alisema aliacha shule kwa mara ya kwanza mwaka
1984 baada ya kuanza na kaka yake aliyemtaja kwa jina la Jugulu.
Mbunge
huyo wa Iramba alisema kutokana na hali hiyo, baba yao aliwataka
wapeane zamu ya kwenda shule hali iliyomfanya aache shule.
“Mwaka
1985, nikaachia darasa la tano nikaenda kuchunga miaka kama miwili.
Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauriwa awekeze
kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi anirudishe
shule, ndiyo nikarudi na nikachukua majina ya daktari.
“Mtu
asichanganye kuona ni udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya mtu.
Nimefanya mitihani tena kwa kupiga na picha za passport ili mtu asitumie
haki ya mtu mwingine aliyefaulu na mpaka sasa naona ni struggle
(kupambana) za mfano, kuwa nilisoma kwa mazingira ya kutoka kuchunga na
kurudishwa shule na kufaulu mwenyewe,” alisema Mwigulu.
Waziri huyo alisema kwa anayetaka kuthibitisha maelezo aliyotoa, anaweza kuwauliza aliosoma nao shule ya msingi.
“Comrades
kwa mawazo yangu kosa ni mtu kuchukua nafasi ya mtu aliyefaulu na
kwenda yeye, hapo ni kuiba haki ya mtu. Najua hii ilikuwa ikitokea
baadhi ya maeneo, mtu anafaulu ila anakuwa hataki kwenda shule au
amefariki then anakwenda mwingine. Mimi sijawahi chukua nafasi ya mtu.
“Halafu
watu wanasema jina la mtu, labda kama wanamaanisha tofauti na wizi wa
jina kwani kila mmoja hapo alipo ana jina la mtu, yaani atakuwa John wa
Biblia, Mohamed wa Quran, litakuwa la babu, bibi la mganga, daktari,
rafiki, kiongozi au hata la tukio.
“Nijuavyo
jina unakula kiapo tu kama sio la kwako kisheria na unatumia, na hata
sasa nikitamani jina jipya nakula kiapo na kutangaza katika Gazeti la
Serikali na lisipopingwa ndiyo linakuwa jina langu jipya.
“Hoja
ni kama mtu kapora cheti cha mtu, kapora nafasi ya mtu mwingine
aliyefaulu akaenda kuisomea yeye. But, things do change pia kutokana na
nyakati na mazingira,” alisema Mwigulu.
Post a Comment