MAHAKAMA YA RUFAA YASHINDWA KUTOA HUKUMU KESI YA UCHAGUZI INAYOWAKABILI ONESMO NANGOLE NA DKT KIRUSWA

Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiongea na waandishi wa habari mara baada ya maamuzi ya rufaa iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo la longine Onesmo Nangole
 
                                                                                             
 Na Woinde Shizza,Arusha

Mahakama ya rufaa kanda ya Arusha imeshindwa kutoa maamuzi ya rufaa iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Longido ,Onesmo Nangole(CHADEMA) ambaye anapinga maamuzi ya mahakama kuu iliyomvua ubunge wake, badala yake imeagiza mwanasheria mkuu wa serikali na msimamizi mkuu wa uchaguzi katika jimbo hilo aunganishwe katika shauri hilo.

Aidha mahakama hiyo imetoa siku 21 kwa mrufani kwa ajili ya kufanya marekebisho ya notisi yake ya rufaa na kuyaleta mahakamani hapo ili msimamizi wa uchaguzi pamoja na mwanasheria mkuu wa serikali waingizwe kama mashaidi muhimu katika rufaa.

Akisoma taarifa ya majaji watatu walikuwa wakisikiliza rufaa hiyo mahakamani hapo Msajili wa mahakama rufaa John Kayanza alisema kuwa mahakama ya rufaa aitatenda haki katika hukumu yake iwapo haita msikiliza mwanasheria wa serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi jimbo la Longido na imewataja kama mashahidi muhimu kwa upande wa mrufani

“kama mahakama itatoa uamuzi bila kusikiliza mwanasheria wa serikali na msimamizi wa uchaguzi haitakuwa imetenda haki katika mahamuzi hivyo mahakama imeonelea ni vizuri mrufani akaifanyie marekebisho notisi yake na ndani ya siku 21 aiwasilishe mahakamani”alisema Kayanza

Katika rufaa hiyo mrufani Onesmo Nangole aliyekuwa mbunge wa jimbo la Longido alikata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama kuu kanda ya Arusha ambayo ilitengua ubunge wake na kuagiza msimamizi wa uchaguzi atangaze jimbo hilo kuwa lipo wazi.

Katika kesi hiyo Onesmo Nangole( CHADEMA) anawakilishwa na mawakili wawili ambao ni Methodi kimomogoro akisaidia na wakili John Materu ambapo kwa upande wa warufaniwa Dkt.Steven Kiruswa (CCM) anawakilishwa na mawakili watatu wakiongozwa na DKT.Masumbuko Lamwai akisaidiwa na Daudi Haraka pamoja na Edmond Ngemela.

Rufaa hiyo inasikilizwa na Majaji watatu ambao ni jaji Sauda Mjasiri,Jaji Musa Kipenka pamoja na Profesa Ibrahimu Juma.

Akiongea mara baada ya kesi hiyo kuairishwa Onesmo Nangole alisema kuwa anaishukuru mahakama kwa kuwapa nafasi na kuona umuhimu wa mwanasheria wa serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi wilayani longido kuja kutoa ushahidi katika shauri hilo na anaamini mahakama hiyo itamtendea haki.

Kwa upande wa Dkt,Kiruswa (CCM) alisema yeye ana tatizo na maamuzi ya mahakama na anaiachia mahakama iendelee kushughulikia shauri hilo na anaamini itatenda haki.

No comments

Powered by Blogger.